Aliyekuwa
daktari wa timu ya Olimpiki Larry Nasser amehukumiwa kwenda jela miaka 175
baada ya kukutwa na makosa ya ukatili wa kingono dhidi wananawake na wana
michezo.
Katika kesi hiyo
mashahidi 160 wamewasilisha ushahidi wao huku Nasser mwenyewe alikiri makosa
kumi.
Alikuwa tayari
akitumikia kifungo cha miaka 60 kutokana na kukutwa na hatia ya kumiliki picha
ngono za watoto kinyume cha sheria.
Jaji Rosemary Aquilina
ameiambia mahakama kuwa amejisikia fahari na furaha kubwa kutoa adhabu hiyo
kutokana na kitendo alichofanya Nasser na kwamba anataka iwe fundisho kwa
wengine.
'Nataka ukae jela
maisha yako yote'. Hata hivyo baada ya hukumu hiyo mmoja wa waathirika
amesisitiza kuwa washirika wa daktari huyo wanapaswa kushitakiwa pia.
Muda mfupi baada ya
kutolewa hukumu hiyo, mkuu wa chuo kikuu cha jimbo la Michigan (MSU) alikokuwa
anafanya kazi Nassar kati ya mwaka 1997 na 2016, amejiuzulu.
Lou Anna Simon amekuwa
akikabiliwa na shinikizo kujiuzulu.
Bi Simon alikana
taarifa kuwa MSU ilifahamu kuhusu tuhuma hizo za unyanyasaji lakini kilishindwa
kuchukua hatua.
Katika taarifa yake
alisema: "kwa waathiriwa, samahani yangu haiwezi kutosha, kuwa daktari
aliyeaminika, aliyefahamika alikuwa ni mtu muovu kwa kweli, aliyewadhulumu kwa
kutumia kigezo cha kuwatibu."
"Ushahidi wa
wahanga wa unayanyasaji wa Nassar ni wa kusikitisha, kuvunja moyo na binafsi
unaonitia kichefu chefu," aliongeza.
Takriban wasichana 140
wamewasilisha kesi dhidi ya Nassar, taasisi ya USA Gymnastics na chuo kikuu cha
MSU, wakidai kuwa taasisi hizo mbili zilipokea tuhuma za unyanyasaji wa kingono
dhidi ya daktarihuyo miaka kadhaa ya nyuma.
Taasisi hiyo ya michezo
na chuo hicho zimekana kuwa kulikuwa na chochote cha kufichwa.
Hukumu ya Larry Naser
inafuatia wiki ya ushuhuda kutoka kwa wanawake takribani mia moja na sitini,
wakiwemo washindi wa medali ya dhahabu ya olympiki Biles, Aly Raisman, Gabby
Douglas na McKayla Maroney
Post a Comment